Mustakbali Mpya?

Miaka nenda, miaka rudi
Tumekuwa tukitaradadi.
Tumeelekea mbele, tumerudi nyuma.
Kuzungukazunguka desturi yetu.

Ramani waliyotupa tunayo mikononi
Lakini yatuelekeza jangwani.
Waliahidi kutufikisha mbuga za peponi.
Leo twajikuta Jehanamu.

Zi wapi hekaheka za madaraka na uhuru?
Ndoto zetu zimekufa.
Bendera zimechakaa, zimeraruka.
Tumeanguka, miguu imevunjika.
Na bado twaimba nyimbo za kale.
Eti twajivunia amani, uhuru na madaraka.

Enzi za ukoloni zimepita,
Lakini kujilisha, kujivisha tumeshindwa.
Eti amani, uhuru na madaraka?
Ndiyo. Amani, uhuru na madaraka;
Madaraka ya vibaraka;
Wanavijiji mafukara wa “Global Village”.

Watoto wa bara wameamka.
Urithi wetu hawautaki, mienendo yetu wanaikana.
Lakini mwana wa nyoka ni nyoka.
Wataujenga upya uafrika?

Creative Commons License This poem is licensed under a Creative Commons Attribution-Noncommercial 3.0 Unported License. Please feel free to use my writing for non-commercial purposes and do credit my name, Rose Kahendi, as the writer.

Comments

Popular posts from this blog

Mgeni siku ya kwanza...

It's time we addressed the ethnic elephant in the room

Salvaging The Help, a film worth watching